KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI IMEKUTANA NA AFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ TANZANIA BARA

 

 

 

 

Kamati ya baraza la wawakilishi inayosimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa imeitaka afisi ya uratibu wa shughuli za smz tanzania bara kufuatilia  utaratibu wa kiitifaki wakati wa mapokezi ya viongozi wakuu wa kitaifa kutoka zanzibar pindi wanapokuwa tanzania bara.

Ni maagizo ya kamati ya baraza la wawakilishi inayosimamamia ofisi za viongozi wa  kitaifa  kupitia kikao chake na wafanyakazi wa ofisi ya uratibu wa shughuli za SMZ dar-es-salaam ikiwa ni katika ziara yake ya siku tano kama  inavyoelezwa na kaimu mwenyekiti  wa kamati hiyo mhe suleiman  shihata.

Akielezea shughuli zilizotekelezwa  katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/19 kaimu mratibu mkuu wa afisi ya smz tanzania bara ndugu alhaji mzare amesema wameshatoa huduma ya usafiri na visa  mara 24 kwa viongozi wa  smz na kuratibu vikao 19 vya wizara na taasisi pamoja na  kutembelea balozi za india, misri  na oman na katika mashirika kadhaa ya kimataifa.

Aidha ndugu mzare akaelezea changamoto ya uhaba wa magari kuwa haulingani na ongezeko la utoaji huduma kwa viongozi  hao wa kitaifa  na kuweza kumudu shughuli zao kama kiungo baina ya wizara na taasisi za muungano na zile za smz.

Kamati ya viongozi wa kitaifa pia imetembelea kwenye makazi ya mhe rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi  jijini dar-es-salaam  ili kujionea hatua ya utekelezaji wa maelekezo iliyoyatoa ya kutaka kufanyika marekebisho  kwenye  makazi hayo ambapo iliridhishwa na maelezo yaliyotolewa na mnikulu  amir ali khatib na kupongeza kamati iliyopita kwa kutoa maelekezo yaliyopelekea kufanyiwa matengenezo kwenye makazi hayo.