KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUVITEMBELEA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI

 

Kamati ya baraza la wawakilishi ikishirikiana na idara ya watu wenye ulemavu wamefanya ziara ya kuvitembelea  vikundi vya ujasiriamali  kwa kuangalia shughuli zinazotekelzwa na mafanikio na changamoto zilizopo.

wajumbe hao  wa baraza hilo wametembelea kikundi cha tumuamini mungu kilichopo kivungewilaya ya kaskazini  kinachojishughulisha na utengenezaji wa makawa mashuka ya kufuma uanikaji wa  madagaa.  Pamoja na kikundi cha  masikini nao watu kinachoshughulikia ulimaji wa mboga mboga.

mkurungenzi idara ya watu wenye ulemavu bi abeida rashid amesema lengo kubwa ni kuwezakuwasaidi wazazi wenye kuwalea  watu wenye ulemavu ili wawezekujikwamua nauchumi badala ya kutegemea misaada peke yake.

Nao wajumbe hao wa baraza la wakilishi wamesema watajitahidi kutatua changamoto zilizopo   ili waweze kupiga hatua za maendeleo na uwataka kusajili akaunti  zao ili kuweza kuzihifadhi  fedha wanazopata za miradi hiyo.

Wanachi hao wanaojishughulisha  na shughuli za ujasiriamali za mboga mboga na ufumaji wa aina mbalimbali za mapambo wameelezea mafanikio na cha ngamoto walizonazo.