KAMATI YA MUDA YA KUSIMAMIA SOKA VISIWANI ZANZIBAR KUWATOA HOFU WADAU WA SOKA

 

Kamati ya muda ya kusimamia soka visiwani zanzibar imewatoa hofu wadau wa soka kwa kufata maagizo makuu waliyopewa ili kukuza mchezo wa soka Visiwani hapa.

Akizungumza na Makatibu na Wenyeviti wa ZFA Wilaya za Unguja pamoja na viongozi wa timu 14 zilizofanikiwa kutinga katika ligi ya mabingwa wilaya, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mwalim Ali Mwalim amesema kamati yao imeundwa kwa mujibu wa sheria na kazi walizopewa watazitekeleza kama wadau wengi wa soka wanavyotaka kuona mchezo wa soka unapiga hatua visiwani hapa.

Nao baadhi ya Viongozi wa Wilaya pamoja na viongozi wa vilabu hivyo wamepata nafasi ya kuzungumza na ZBC.

Nae katibu wa kamati hiyo Khamis Abdallah Said ametoa shukrani kwa wadau hao wa soka ambapo wamefikiana kuanza ligi ya mabingwa wilaya Agost 5, 2018 kwaajili ya kuzitafuta timu zitakazopanda daraja kutoka la pili wilaya mpaka la 2 taifa ambapo kwa leo tayari imepangwa makundi manne.

Hivi karibuni ofisi ya mrajis wa vyama vya michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza ameifungia kamati tendaji ya ZFA na kuunda kamati hiyo ambayo imepewa kazi kuu ya kusimamia upatikanaji wa katiba mpya ya ZFA, kusimamia ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora, ligi ya mabingwa Wilaya, pamoja na kusimamia majukumu yote ya kikatiba ya kamati tendaji.