KAMPUNI YA ZANTEL IMEKAMILISHA MRADI WA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZAKE

 

 

Kampuni ya  huduma  za mawasiliano  ya zantel  imekamilisha  mradi  wa  kuimarisha  miundombinu  ya  huduma  zake  uliogharimu  dola  kimarekani  milioni  nne   nukta  tatu.Kufuatia  kukamilika  kwa  mradi  huo  kampuni  hiyo  imezindua  kampeni  mpya inayojulikana  kwa   jina la Tunaliamsha  kivingine  yenye  lengo la  kuwawezesha wateja  wa  zantel  kupata  huduma  bora   na  viwango .Akizungumza   katika  uzinduzi  wa  kampeni  hiyo  meneja  wa   zantel   kanda  ya  Zanzibar   nd.  Khamis  Baucha amesema  kwa  miaka  miwili  kampuni  hiyo  imejikita  katika  kuhakikisha  huduma  zake  zinaimarika  ili  kuweza  kuhimili   ushindani  katika  utoaji  wa  huduma kwa wateja  nchi nzima. kampeni  hiyo  ya  tunaliamsha  kivingine  inajumuisha   vifurushi  maalum  vya  data  vitakavyowawezesha  wateja kutizama  mechi  za  kombe  la  dunia  nchini  Urusi  kwa  ufanisi  mkubwa na  kwa   gharama nafuu zaidi.Nd.  Baucha  amewahakikishia  wateja  wa  zantel  kuwa  itaendelea  na kwenda  na  kasi  ya  mabadilko  ya  teknologia  ya   mawasiliano  duniani  ili   kuwaridhisha  wateja   kuwa  na  huduma   zenye  sifa   na  viwango  vya  ubora.