KAMPUNI ZINAZOJISHUGHULISHA NA UUZAJI NA UTENGENEZAJI WA VIFAA VYA ZIMAMOTO KWENDA KUJISAJILI

Kikosi cha zimamoto na uokozi kimetoa muda wa wiki mbili kwa kampuni zote zinazojishughulisha na uuzaji na utengenezaji wa vifaa vya zimamoto kwenda kujisajili ili kupewa taratibu sahihi za kuendesha kazi hizo.
Agizo hilo linafuatia kubaini watu wengi kufungua kampuni hizo bila ya kufuata sheria na kufanya udanganyifu katika kazi zao jambo linaloweza kuleta athari kubwa hapo baadae.
Naibu kamishna wa zimamoto gora haji gora akizungumza na wamiliki wa kampuni hizo pamoja na maafisa wa jeshi hilo amesema watafuatilia wale wote wanaojihusisha na mambo hayo kinyume cha sheria na kuhakikisha hali ya usalama katika masuala ya zimamoto.
Aidha amewataka wafanyakazi wa jeshi hilo waache kujihusisha na masuala hayo ili kuepusha kulitupia lawama jeshi hilo pale linapotokezea tatizo.
Ametoa wito kwa taasisi za serikali na binafsi zinazohitaji huduma hizo kufuata taratibu kabla ya kununua vifaa hivyo.