KASI YA MAENDELEO HAYAWEZI KUFIKIWA BILA KUWEPO USHIRIKIANO WA VIONGOZI

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Samia suluhu hassan amesema kasi ya maendeleo ya sehemu yeyote hayawezi kufikiwa bila kuwepo ushirikiano wa viongozi na serikali katika kutatua kero za wanananchi.
Akizungumza na katika sherehe siku ya wananchi ya kizimkazi yaliyofanyika kijiji cha kizimkazi mkunguni amesema bila ya viongozi kuweka kipaumbele hicho dhana ya kustawisha maisha ya jamii haitafikiwa kama inavyosisitizwa na serikali.
Amewataka wananchi kuwa na mikakati ya pamoja ya kuandaa vipaumbele vitakavyotekelezwa kuanzia ngazi ya chini kama hatua ya kujenga ari ya viongozi kushirikiana nao.
Akizungumzia tatizo la nyumba ya walimu, madaktari pamoja na vyoo vya skuli katika kijiji hicho cha kizimkazi mh. Samia amesema atasaidia kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Aidha ameahidi kuwalipia bima ya afya wananchi wenye vigezo maalumu ili kuwaondoshea matatizo ya kupata huduma za matibabu kwa urahisi.
Mkuu wa mkoa wa kusini unguja dk. Idrissa muslim hija amesema serikali imeendaa mikakati zaidi ya kuimarisha maendeleo zaidi ambapo pia na wananchi wameelezea kuridhishwa na hatua za maendeleo kijijini hapo.