KASKAZINI PEMBA IMEREJEA ZANZIBAR IMESHIKA NAFASI YA TATU

 

Timu ya Mkoa wa kaskazini pemba imerejea zanzibar ikishika nafasi ya tatu katika Mashindano ya Mikoa Tanzania kwa upande wa Wanawake yaliyomalizika jana jijini Dar es salam.

Akizungumzia Mashindano hayo mara tu walipowasili Bandarini Unguja  nahodha wa Zanzibar Kazija Hassan Simai amesema mashindano yalikuwa magumu lakini wao walishindana kadri ya uwezo wao mpaka wakafanikiwa kushinda nafasi ya tatu.

Nae mchezaji Lulu Richard kutoka Mkoa wa Kazkazini Pemba ambae ni mrushaji wa tufe na kisahani yeye ameshinda medali ya dhahabu na fedha na hapa akielezea ushindi huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama amesema Zanzibar Mashindano yalikuwa magumu lakini anawapongeza vijana wake kwa kushinda nafasi ya tatu.

Lengo la Mashindano hayo ni kuwapata wanariadha bora katika Mashindano ya Olimpik yatakayofanyika Tokyo nchini Japani mwaka 2020 huku Wazanzibar baadhi wao wakitarajiwa kushiriki kutokana na kufanya vyema.