KASSIM MAJALIWA AMETEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA SAMAKI

Waziri mkuu kassim majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika samaki aina ya jodari na kuwakaribisha viongozi wa kiwanda hicho kuja nchini kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya samaki.
Amesema serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji na pia ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya samaki, ambayo ni bahari, mito na maziwa ambayo ina aina mbalimbali za samaki.