KENYA KUSHIRIKI UCHAGUZI MPYA NDANI YA SIKU 60

Wagombea wa urais nchini kenya wanajiandaa na uchaguzi wa marudio baada ya mahakama ya juu nchini humo kubatilisha matokeo ya uchaguzi hapo jana.
Mahakama hiyo imeamuru uchaguzi huo ufanyike ndani ya siku sitini na imesema itatoa ufafanuzi ndani ya siku 21 kuhusu sababu za kufuta uchaguzi huo.
Hata hivyo mahakama hiyo imeonyesha ukosoaji mkubwa kwa tume huru ya uchaguzi nchini kenya kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa mwezi agosti.
Wakati huo huo rais uhuru kenyata amesema hakuridhishwa na uamuzi huo lakini amesema atashiriki uchaguzi wa marudio ambao unatakiwa ufanyike ndani ya siku sitini kuanzia siku ya uamuzi.