KERO NYINGI ZINAWAKABILI WANANCHI KATIKA BIASHARA YA UTALII HASA KWENYE HOTELI

 

 

Tume ya haki za binadamu na utawala bora, imesema imebaini kero nyingi zinazowakabili wananchi katika biashara ya utalii hasa kwenye  hoteli.

Kamishana wa tume hiyo mohammed hamed amesema  katika utafiti mdogo walioufanya hivi karibuni wamabaini baadhi ya wananchi wanashindwa kutumia fukwe, wanakosa huduma muhimu za kijamii na wanakumbwa vitendo vya unyanyasaji utoka kwa walinzi wa hoteli .

Akizungumza katika warsha ya haki za binaadamu na biashara amesema licha ya kuwa sekta hiyo kuwa na nafasi ya kukuza uchumi ila ni muhimu kuzinagitia haki za jamii katika kazi zao.

Naibu katibu mkuu katiba na sheria, kubingwa mashaka simba,  akizungumza katika warsha hiyo amesema serikali   itaendelea kulinda na kuitetea jamii ili kujenga uhusiano mzuri na wananchi wake.

Ambapo amesema katika kuhakikisha hilo mikakati kadhaa imetayarishwa kudhibiti hujuma zinazofanywa na wawekezaji ili kuepusha migogoro itakayoathiri jamii na sekta hiyo.