KIASI CHA HEKTA ELFU MOJA ZA MISITU ZINAKATWA KILA MWAKA

Naibu waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mhe, makame ali ussi  amesema kasi ya ukataji wa misitu isiyolingana na upandaji wa miti mingine huenda ikapoteza kabisa rasilimali hiyo katika visiwa vya unguja na pemba.Amesema takwimu zinaonesha kwamba kiasi cha hekta elfu moja za misitu zinakatwa kila mwaka huku upandaji wa miti ukiwa ni hekta mia sita na hamsini na mbini tu kwa mwaka kiwanga ambacho ni kidogo mno.

Akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya siku ya misitu duniani huko masingini  mhe, ussi amesema ujezi wa maofisi,makazi vuiwanda na miundombinu  lazima uzingatie umuhimu wa kuwepo kwa mkisitu nchini.Amesema wizara yake itaendelea kazi ya upandaji miti ya asili na matunda  na kudhibiti ukataji ovyo wa miti na kuwataka waandishi wa habari kuisaidia serikali kuhamasisha wananchi kupnda miti  kwa wingi ili kurejesha hadhi ya zanzibar ya kuwa visiwa vya kijani.

Naibu katibu mkuu katika wizara hiyo ndugu ahmad kassim  amesema wakati umefika kwa rasilimali ya msitu zanzibar kulindwa kwa kila hali hasa ukizingatia  inachangia pato la taifa kutokana na kutembelewa na watalii.Mkurugenzi wa idara ya maisitu na rasilimali zisizorejersheka ndugu soud mohammed juma amesema vyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kuimarisha kampeni ya upandaji miti kwa vile vinaaminiwa na jamii.   Kilele cha siku ya misitu duniani hapa zanzibar kitafanyika  tarehe 21 mwezi huo katika  ukuimbi wa zamani wa baraza la wawakilishi zanzibar kikwajuni