KIASI YA WATU 18 WAMEUWAWA NA WENGINE 29 KUJERUHIWA BAADA YA WATU WANNE WA KUJITOA MUHANGA

 

Kiasi ya watu 18 wameuwawa na wengine 29 kujeruhiwa baada ya watu wanne wa kujitoa muhanga kujiripua kaskazini mashariki mwa nigeria.

Mripuko wa mwanzo umetokea siku ya jumatano jioni katika sehemu ya ibada katika kitongoji cha munagari nje kidogo ya mkoa wa maiduguri na miripuko mengine imetokea katika mitaa jirani.

Msemaji wa polisi amesema katika watu hao 18 waliokufa ni pamoja waripuaji wanne katika mfululizo huo wa mabomu.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya chuo kikuu cha maiduguri na hospitali ya taifa kwa uchunguzi zaidi.

Na ameongeza kuwa polisi na timu za kunasua mabomu wanafanya doria katika maeneo ya matukio.

Hadi sasa hakuna kundi lililotaja kuhusika lakini kundi la boko haram ndio linahusishwa zaidi na matukio hayo.