KIASI YA WATU SITA WAMEUAWA BAADA YA MSHAMBULIAJI WA KUJITOA MUHANGA KUJIRIPUA

 

Kiasi ya watu sita wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujiripua katika maeneo ya idara ya ujasusi mjini kabul nchini afghanistan katika shambulizi  linalodaiwa kufanywa na kundi la itikadi kali linalojiita dola la kiisilamu (is).

Mshambuliaji amefanya shambulizi hilo wakati wafanyakazi walipokuwa wakiwasili katika ofisi za idara hiyo ya kurugenzi ya usalama wa taifa, ikiwa ni wiki moja baada ya washambuliaji wengine kuvamia kituo cha mafunzo ya usalama  mjini kabul.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani najib danish  amesema kuwa raia sita waliokuwa katika gari wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa wakati mshambuliaji huyo alipojitoa muhanga.