KIJANA WA KITANZANI AAMEIBUKA KIDEDEA KATIKA MASHINDANO YA QURAN

 

Kijana wa kitanzania, shujaa suleiman shujaa ameibuka kidedea na kitita cha sh. Milioni 15 katika mashindano ya 19 ya afrika ya kuhifadhi quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa morogoro, amejishindia pia laptop, kiwanja chenye hati eneo la kigamboni kilichotolewa na kampuni ya property international ya jijini dar es salaam pamoja na dola za marekani 500.Akizungumza na maelfu ya waumini na watanzania katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam waziri mkuu kassim majaliwa amewataka watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada.

Amesema katika nchi ambazo amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa kujificha hivyo ni fursa adhimu kwa watanzania kuienzi amani iliyopo.katika hatua nyingine, waziri mkuu amemtaka sheikh nurdin mohammed (kishki) akaonane na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la matumbi ambacho mwaka jana aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe. Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni ahmed noor wa sudan akifuatiwa na muzamil awadh mohamed wa sudan. Washiriki wengine ni kutoka nchi za rwanda, burundi, msumbiji djibouti, kenya, ethiopia, congo drc, nigeria, ghana na afrika kusini.