KIKAO CHA PAMOJA BAINA YA OFISI YA MUFT MKUU WA TANZANIA NA MUFT MKUU WA ZANZIBAR

Kikao cha pamoja baina ya ofisi ya muft mkuu wa tanzania na muft mkuu wa zanzibar kimefanyika jijini dar-es-salaam ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya ushirikiano baina ya pande mbili za jamhuri ya muungano.

Akizungumza na zbc muft mkuu wa tanzania shehe abubakar zuberi bin ali amesema kikao hicho kimewahusisha mashehe wanaofungamana na ofisi ya muft wa tanzania bara na wale wa ofisi ya muft mkuu wa zanzibar.

akifafanua agenda za kikao shehe zuberi amesema pamoja na mambo mengine pia wameweza kuzungumzia masuala ya hija ili kurekebisha kasoro ama za kimfumo ambazo zilipelekea kuleta usumbufu kwa kuwachelewesha baadhi ya mahujaji na kukwama wengineo katika kushiriki  nguzo hiyo muhimu ya uislamu.

Naye muft mkuu wa zanzibar shekhe saleh kambi ametaja madhumuni,  kujadili mambo yanayowahusu waislaamu wa tanzania ili kwenda sambamba katika nia moja na kuendeleza mambo mazuri na kuweka amani ya kudumu na kutokuwapo na ubaguzi kwa baina ya waislaamu na kwa wasio waislaamu.

Akifafanua maazimio ya kikao hicho katibu wa muft zanzibar shehe suleiman khamis soraga ameelezea baadhi ya mambo yaliyojadiliwa.