KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANI

Serikali inaendelea kuwajengea uwezo wananchi katika kutumia fursa za mikopo na kuongeza kasi ya kutafuta masoko ili kuona wakulima wa mwani wanaongeza uzalishaji na ubunifu.
Hatua hiyo italeta tija kwa wakulima wa kilimo hicho kilichoanza kulimwa nchini kwa miaka mingisasa ili kujikwamua kiuchumi na kukuza mapato.
Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi alitoa kauli hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mwani ya kongano bunifu la mwani zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya michezo vya malindi mjini zanzibar.
Balozi seif alisema mwenendo wa mapato kwa wananchi unaonekana kuongezeka siku hadi siku na kuonyesha haja kwa serikali kuendelea kutilia mkazo uzalishaji wa zao mwani kwa vile ni sekta ya tatu kwa kuleta tija kwa taifa ikitanguliwa na utalii na karafuu na ni zao la pili kwa kusafirishwa nje ya nchi likitanguliwa na karafuu.
Alisema sekta hiyo tayari imeshatoa ajira za kudumu kwa zaidi ya wakulima 23,000 na kuna ajira nyingi ambazo hutokea kipindi cha msimu wa kupanda, kuvuna na kusarifu mwani.
Alieleza kwamba faida imeanza kuonekana kupitia zao la mwani kiuchumi ambapo wananchi kutoka vijiji mbali mbali vya zanzibar na hata baadhi ya wilaya za tanzania bara walijishughulisha na zao hilo ambapo asilimia kubwa ya wakulima wake ni akinamama.
Amempongeza mwenyekiti na mwezeshaji wa kongano la mwani dr. Flower msuya kwa uwamuzi wake wa kushirikiana na wizara ya kilimo zanzibar pamoja na shirika la milele foundation zanzibar kuwa bega kwa bega na wakulima katika kuzitambua changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Mapema mwenyekiti na mwezeshaji wa kongano la ubunifu wa mwani dr. Flower msuya alisema bidhaa za mwani hivi sasa zimefikia 50 ikilinganishwa na bidhaa moja tuu iliyokuwa ikizalishwa na kikundi cha tusife moyo cha kijiji cha kidoti mnamo mwaka 2006.
Dr. Flower alisema mipango ya baadae ya ya taasisi hiyo ni kuendelea kutengeneza bidhaa zinazotokana na zao la mwani baada ya kufanyiwa utafiti uliothibitisha kwamba bidhaa hiyo ina matumizi mengi mchanganyiko ikiwemo chakula.
Akitoa salamu za taasisi ya milele zanzibar foundation iliyoratibu hafla hiyo ya siku ya mwani duniani, mwakilishi wa milele zanzibar bibi khadija sharifu alisema taasisi yake inakusudia kuwaleta wataalamu wa kigeni kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wazalishaji wa mwani.
Bibi khadija alisema wataalamu wa milele wamegundua kwamba sekta ya mwani inaweza kuwakomboa wananchi walio wengi kwa kutoa ajira kubwa ambapo kwa sasa tayari imetoa ajira ya watu zaidi ya 23,000 tokea kuanza kwa sekta hii nchini tanzania.
Akimkaribisha mgeni rasmi kwenye siku hiyo ya mwani duniani waziri wa kilimo, mali asili, mifugo na uvuvi zanzibar mheshimwa hamad rasid mohamed alisema jamii inapaswa kubadilika katika utaratibu wao wa lishe na kupoenda kutumia mazao ya mwani kwa lengo la kujenga afya zao.
Waziri rashid alisema zao la mwani kwa utafiti wa kitalaamu linaonyesha kukinga maradhi mbali mbali ikiwemo ukanda wa jeshi, mshtuko wa moyo pamoja na maradhi yanayodhoofisha upungufu wa damu kutokana na ulaji ovyo wa vyakula vya makopo.
Mapema makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif alipokea maandamano ya wazalishaji wa zao la mwani kutoka wilaya mbali mbali za unguja na pemba na baadaye kukagua bidhaa zao wanazozalisha kutokana na mali ghafi hiyo ya mwani.
Wakulima hao walimueleza balozi changamoto wanazopambana nazo katika harakati zao za kulima zao hilo kukausha hadi kukamilika kwa ajili ya soko ambapo walisema kodi ya bidhaa iwanayotozwa kuhusiana na bidhaa ya zao hilo
Zao mwani limekuwa likitumika kwa kutengeneza sabuni, mafuta ya kujipaka, shampuu na vyakula vya kama juisi keki, jam, kachumbari na kupikwa kama mboga sambamba na utengenezaji wa dawa za binaaadamu, vipodozi na chakula cha mifugo.
Ujumbe wa mwaka huu wa siku ya mwani duniani unaeleza mwani kwa afya, mwani kwa kipato na mwani kwa uwezeshaji.