KILELE CHA SHEREHE YA KIZIMKAZI DAY KATIKA FUKWE YA KIZIMKAZI MKUNGUNI.

 

Nahodha nassor ali amefanikiwa kushinda katika resi za ngarawa baada ya kuwapita wenzake katika mashindano ya kilele cha  sherehe ya kizimkazi day katika fukwe ya kizimkazi mkunguni.

Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania, samia suluhu hassan alivutiwa mno na resi hizo ambapo captain nassor aliwashinda wenzake tisa akiwemo masoud hassan aliyekamata nafasi ya pili.

Mara baada ya kumaliza mchezo huo zbc michezo walipata nafasi ya kuzungumza na wanamichezo hao.

Mbali ya resi za ngalawa katika mashindano hayo ya kilele cha  sherehe ya kizimkazi, pia kulichezwa michezo mbali mbali ikiwemo soka, mpira wa pete na kuvuta kamba.