Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean

 

 

Kimbunga kikali kilichoitwa jina irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la caribbean ambapo kiasi watu saba wameuawa.

Kisiwa kidogo cha barbuda kinaarifiwa kuharibiwa vibaya hadi kutajwa kuwa kisiweze  kukalika pamoja na eneo la himaya ya uingereza ya st martin imeharibiwa kabisa na bado kuna ugumu wa jitihada za uokoaji katikabaadhi ya maeneo.

Zaidi ya nusu ya wakaazi wote milioni tatu wa puerto rico hawana umeme baaada ya kimbunga irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.

Kimbunga hicho chenye nguvu nyingi kuwai kushuhudiwa kwa miongo kadha kilikuwa na upepo wa kasi ya kilomita 295 kwa saa na kimepita karibu na pwani cha jamhuri wa dominica.