KIOGOZI MKUU WA KANISA KATOLIKI DUNIANI PAPA FRANCIS AMETOA SALAAM ZAKE ZA KRISMASI

 

Kiogozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis   ametoa salaam zake za krismasi na kutoa wito kwa waumini kiasi ya bilioni 1 wa kanisa katoliki duniani kutopuuza hali inayowakabili wakimbizi ambao wanalazimika kuyahama makazi yao kwa sabababu mbali mbali.

Papa francis amewaeleza waumini katika mkesha wa krismasi katika kanisa la mtakatifu petro kuwa ulimwengu umekuwa ukishuhudia mamilioni ya watu wakihama makazi yao na kuwaacha raslimali zao na wapendwa wao.

Amesema wengi wanaokumbwa na hali hiyo wanalazimika kuwa wakimbizi kutokana na viongozi wenye tamaa ya mali na madaraka ambao hawajali kumwaga damu ya watu wasio na hatia.

Ujumbe huo wa papa katika mkesha wa krismasi umekuja  wakati mivutano mipya ikiibuka katika ukingo wa magharibi kufuatia rais donald trump kutangaza kuitambua jerusalem kama mji mkuu wa israel huku pia rais wa guatemala jimmy morales akisema nchi yake itahamishia ubalozi wake mjini humo.