KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE AMEUNGANA NA WASHIRIKA WAKE WA ZAMANI

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini zimbabwe morgan tsangirai ameungana na washirika wake wa zamani ili kukabiliana na rais robert mugabe katika uchaguzi wa mwakani.
Tsvangirai anaeongoza chama cha upinzani cha mdc amesema ameamua kuungana na manaibu wake wawili waliokuwa pamoja katika serikali ya awamu iliyopita ya mseto kuanzia mwaka 2009 hadi 2013.
Miongoni mwawatakaounda muungano huo mpya wa upinzani ni welshman ncube na mpambe wake wa karibu tendai biti pamoja na mkuu wa chama cha zimbabwe people first agrippa mutambara.
mugabe mwenye umri wa miaka 93 ameliongoza taifa hilo koloni la zamani la uingereza tangu uhuru wake 1980.