KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI PAPA FRANCIS ANAFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA MYANMAR

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa francis anafanya mazungumzo na kiongozi wa myanmar suu kyi, hiyo ikiwa sehemu muhimu ya ziara yake nchini myanmar, inayolenga kutuliza chuki za kidini na kikabila, ambazo zimesababisha idadi kubwa ya warohingya waislamu kuitoroka myanmar kuelekea bangladesh.

Mkutano huo unaofuatiliwa kwa karibu, unajiri wakati suu kyi ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya nobel akiwa ametengwa na makundi ya kutetea haki za binadamu duniani.

Makundi ya kutetea haki za binadamu hayakuridhishwa na hatua za kiongozi huyo za kusuluhisha suala la mateso ya warohingya.

Baada ya mazungumzo yao, papa francis atatoa hotuba yake ya kwanza mbele ya suu kyi pamoja na wanadiplomasia  kuhusu machafuko ya myanmar.

Hapo jana, papa francis alitembelewa na mkuu wa majeshi ya myanmar ambaye umoja wa mataifa na marekani zinaamini ameongoza kampeni ya mauaji ya kikabila dhidi ya warohingya katika jimbo la rakhine.