KIONGOZI WA NCHI HIYO KIM JONG UN AMEAMURU UTENGENEZAJI ZAIDI WA MAKOMBORA IMARA YA KIVITA.

 

Televisheni ya korea kaskazini imesema kiongozi wa nchi hiyo kim jong un ameamuru utengenezaji zaidi wa makombora imara ya kivita.

Wakati wa ziara yake katika taasisi inayotengeneza vifaa vya kemikali ya chuo cha mafunzo ya sayansi ya ulinzi kim amefahamishwa juu ya hatua za utengenezaji wa makombora ya kivita yanayoweza kuvuka mabara.

wakati huo huo vikwazo vipya vya marekani vilivyotangazwa vinalenga makampuni ya china na urusi, pamoja na watu binafsi, kwa kusaidia mpango wa silaha za nyuklia wa pyongyang.