KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI URUSI AKAMATWA

 

 

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini urusi alexei navalny, amekamatwa baada ya kutokea kwa maandamano makubwa ya kutaka kujiuzulu kwa waziri mkuu dmitry medvedev mwishoni mwa wiki iliyopita jijini moscow.

Maelfu ya wanaandamanaji walijitokeza kuandamana wakidai kujiuzulu waziri mkuu huyo kwa madai ya ufisadi katika serikali yake.

Maandamano hayo yalizua makabiliano makali katika miji mbalimbali nchini humo kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Navalny anayepanga kuwania urais mwaka 2018, ni miongoni mwa waandamanaji 5000 waliokamatwa katika miji mbalimbali nchini humo.

Marekani na muungano wa umoja wa ulaya wamelaani kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani na waandamanaji wengine