KITOPE KINATARAJIWA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI

 

 

Kituo cha afya kitope kinatarajiwa kunufaika na huduma ya maji baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kisima ambacho kitamaliza usumbufu wa muda mrefu wa kupatikana kwa huduma hiyo.

Kituo hicho ambacho kinatoa huduma za kujifungulia wajawazito kimekuwa na ukosefu wa huduma ya maji hali inayolazimu kinamama hao kuchukuwa maji kutoka nyumbani kwao kwa ajili ya kuyatumia wakiwa kituoni hapo.

Diwani wa wadi ya mbaleni hassan ameir  amebainisha kuwa matumaini ya kupatikana maji katika kituo hicho pamoja na maeneo jirani kitawapa faraja ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora kwa wananchi na katika maeneo karibu badala ya kufuata huduma katika hospitali za rufaa.

Upelekaji wa huduma ya maji katika kituo hicho ni utekelezaji wa ahadi ya naibu katibu mkuu wa ccm zanzibar dk. Abdalla juma mabodi kufuatia maombi ya wakaazi wa eneo hilo ambapo msimamizi wa ujenzi wa kisimahicho ramadhan ali amewataka wananchi washirkiane kuona mradi huo unakamilika kwa wakati.