KITUO CHA AFYA CHA SEBLENI KINAKABILIWA NA MATATIZO YA UHABA WA VIFAA NA WAFANYAKAZI

 

Kituo cha afya cha sebleni kinakabiliwa na matatizo ya   uhaba wa vifaa na wafanyakazi hali inayorejesha nyuma utoaji wa baadhi ya huduma katika kituo hicho.

Wakizungumza na mkuu wa wilaya pamioja na naibu mkurugenzi wa baraza la manispaa  mjini katika  ziara ya kuangalia utendaji wa kazi pamoja na kujua  matatizo yanayoikakabili  hosipali ya kwa wazee wamesema tatizo hilo  ni la kipindi kirefu sasa.

Wamesema kutokana na kukua kwa majukumu ya kituo hicho kufikia daraja la pili huduma nyingi zimerejeshwa vituoni kama  uzalishaji na usafishaji kwa walioharibu ujauzito na huduma za kisukari na hiv.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya mjini bi marina joel thomas  amesema ameridhwa  na huduma za hospitali  hiyo licha ya changamoto ndogo ndogo zinazo wakabili.

Kituo cha afya cha sebleani  kinakisiwa kupokea wagojwa wapatao 150  kwa siku na  kuzalisha wazazi kiasi cha  50 kwa mwezi.