KITUO CHA MAFUTA KINACHOMLIKIWA NA KAMPUNI YA UNITED PETROLEUM KIMEUNGUA MOTO

Kituo cha mafuta cha kinazini kinachomlikiwa na kampuni ya united petroleum kimeungua moto

Visima yake ya kuhifazia mafuta nakusababisha kiwanda cha mbao kilichokaribu yake kuteketea kwa moto
Moto huo uliosababishwa na gari la mafuta lilofika kwa ajili ya kumimina mafuta kituoni pia umeteketeza gari hilo pamoja na kuteketeza kisima cha mafuta kituoni hapo.
Akizungumza kwenye tukio hilo kamishina msaidizi wa kikosi cha zimamoto zanzibar gora haji gora moto huwo umezibitiwa na vikosi vyote vya ulizi japokuwa haikuwa rahisi kwa tukio kubwa kama hilo .
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa mjini magharib hasani nasiri amewapongeza vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi walio shirikiana kwenye tukio hilo.
Mkuu wa wilaya mjini amesema katiko tukio hilo ipo haja ya kukanao pamoja kati ya wamiliki wa kituo cha mafuta na wamiliki wa cha mbao
Miongo mwawalio athirika na tukio hilo wameweza kielezea tukio hilo
Walioshuhudia wamesema gari ndio chanzo cha moto huo
Kamishina wa zimamoto ametowa rai zake kuhusu vituo vya sheli kuwa na vifaa vya kisasa kuliko walivyo kuwa navyo.