KITUO CHA MAKONGENI LANGUAGE CENTRE KUFUNGUA MAKTABA ITAKAYOWASAIDIA WANAFUNZI KUPATA TAALUMA

afisa mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya amali pemba salim kitwana sururu amekitaka kituo cha makongeni language centre kufungua maktaba itakayowasaidia wanafunzi kupata taaluma akizungumza katika mahafali ya 7 ya wanafunzi waliohitimu mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa kipindi cha miezi tisa afisa mdhamini huyo amesema vitu vingi katika ulimwengu wa kisasa vinahitaji lugha ya kiingereza na wanafunzi wengi wanashindwa kujieleza , kuandika na kujiamini kwa kutumia lugha hiyo , hivyo kuwepo na library na kufanya midahalo ya mara kwa mara kutaongeza ujuzi wa kutumia ya kiingereza.
katika risala ya wahitimu hao wamesema wamefaidika na mafunzi hayo kwani yamewajengea uwezo wa kushiriki katika mambo mbalimbali ndani na nje ya zanzibar na kukitaka kituo hicho kuanzisha mafunzo ya lugha nyengine ili kupata upeo zaidi baadhi ya wazazi walikuwa na haya ya kusema