KIWANGO KIDOGO CHA DAMU HAPA ZANZIBAR MWEZI WA RAMADHAN

 

Taasisi zinazochangia damu zimesema zinalazimika kuomba damu kutoka tanzania bara  katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa sababu ya kukusanya  kiwango kidogo cha damu kisichokidhi mahitaji hapa zanzibar.

Wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwa wakaazi wa wilaya ya kaskazini ‘b’ ikiwa na lengo la  kuchangia benki ya damu ambayo imekuwa na upungufu kufuatia kuwepo na idadi kubwa ya wahitaji, katibu wa  jumuiya ya kuchangia damu zanzibar nd. Bakari hamadi mbarawa na makamo mwenyekiti wa taasisi  ya g1 nd. Ramadhan ali wamesema tatizo la upungufu wa damu litapatiwa ufumbuzi.

Taasisi ya kiserikali inayojishughulisha na huduma za kijamii,  g1 kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya kaskazni  ’b’ imeendesha  zoezi la kuchangia damu kwa wakaazi wa wilaya ya kaskazini  “b” ikiwa na lengo la  kuchangia benki ya damu ambayo imekuwa na upungufu kufuatia kuwepo na idadi kubwa ya wahitaji.

Baada ya kushiriki zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika katika wilaya zote za unguja na pemba, mkuu wa wilaya ya kaskazini ‘b’ nd. Rajab ali rajab amewataka wakaazi na wananchi kuitumia vyema fursa hiyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine

Baadhi ya waliochangia damuzoezi hilo wamefarajika kwa kuwa ni  miongoni mwa walishiriki kuokoa maisha ya wengine na kutambua afya zao kiujumla

Zoezi hilo limeendeshwa na taasisi ya kiserikali inayojishughulisha na huduma za kijamii,  g1 kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya kaskazni  ’b’