KMKM KAMBI YA KIZIMKAZI IMEFANIKIWA KUKAMATA BIDHAA MBALI MBALI ZA MAGENDO HUKO KATKA MAENEO PUNGUME

 

Kikosi maalum cha kuzuwia magendo kmkm kambi ya kizimkazi imefanikiwa kukamata bidhaa mbali mbali za magendo huko katka maeneo pungume wakati walipokua katika doria yao ya kawaida

Akizungumza mara baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo kamanda wa zone ya kizimkazi hassan bakari babu amesema kua magendo hayo yamekamatwa majira ya saa nne usiku yakitokea kisiwani uzi na kupelekwa dar esslam

Kamanda huyo amesema kua wananchi wa kisiwa cha uzi wanajishughulisa sana na biashara za magendo hivyo ni vyema kwa wakati huu kutafuta kazi nyengine za halali zitakazowaingizia mapato kuliko kufanya biashara hiyo haramu

Nae mkuu wa wilaya kusini idrisa kitwana mustafa amesema kua serikali ya wilaya haitomvumilia mtu yoyote anaejishugulisha na biashara hiyo na yoyote atakae kamatwa atafikiswa katika vyombo vya sheria na kufunguliwa mashtaka pamoja na kutaifishwa mali yote inayokamatwa

Waliokamatwa na biashara hiyo haramu ni pamoja na ramadhan khamis ambae ni nahodha, haji shomari na haji khamisi wote ni wakaazi wa kisiwa cha uzi ambao wamekamatwa na sukari pacti 70 , mafuta ya kupikia, vifaa vya mziki, baiskeli pamoja na mafriza.