KMKM KIZIMKAZI IMEKAMATA BOTI MBILI ZILIZOPAKIA BIDHAA ZA MAGENDO

Kikosi cha kuzuia magendo kmkm kizimkazi kimekamata boti mbili zilizopakia bidhaa mbali mbali kwa ajili ya kusafirishwa tanzania bara kwa njia ya magendo.

Bidha hizo ni pamoja na  sukar pkt 189, kanga katuni tano,simu za mkokoni  katoon 4 na madumu 200 ya mafuta ya kula.

Akithibitisha kukamatwa kwa bidhaa hizo mkuu wa kambi hiyo kamanda hassan bakari babu  amesema bidhaa hizo zilikamatwa majira ya saa kumi na mbili za jioni wakati askari walipokuwa wakifanya doria zao za kawaida maeneo ya bahari ya kizimkazi na kuzibaini boti hizo ambazo ndani yake zilikuwa zimebeba mzigo huo.

Amewataka wananchi kuachana na tabia za kusafirisha bidhaa zao katika bandari zisizo rasmi ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza.

Mkuu wa wilaya ya kusini mhe idrissa kitwana mustafa ambae alifika katika kambi hiyo amewapongeza maofisa na wapiganaji wa kikosi hicho kwa juhudi zao wanazozichukuwa katika kupambana na vitendo hivyo vinavyopelekea kuhujumu uchumi wa nchi na kuagiza

kuzipandisha juu boti hizo mara moja.