KONGO IMEYABAINI ZAIDI YA MAKABURI KUMI YA PAMOJA KATIKA MKOA WA KASAI

Mamlaka nchini jamhuri ya kidemokrasia ya kongo imesema imeyabaini zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa kasai eneo lilofanyika mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia.
Mwendesha mastaka wa kijeshi generali joseph ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa kamuina nsapu wanapigana na majeshi ya serikali.
wiki iliyopita umoja wa mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea katika mkoa huo wa kasai ambapo kiasi watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu na tayari umoja huo umelionya jeshi la taifa la kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.