KOREA KASKAZINI IMEFANIKIWA KUFANYA JARIBIO LA BOMU LA HYDROJENI

Korea kaskazini imesema imefanikiwa kufanya jaribio la bomu la hydrojeni ambalo ni aina ya bomu la kinyuklia la kiwango kikubwa. Umoja wa mataifa umeutaja mpango huo wa kinyuklia wa korea kaskazini kuwa unaleta wasiwasi mkubwa baada ya taifa hilo kufanya jaribio lake la sita la kinyuklia tokea mwaka 2006.
Shirika la mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia, ctbto, limesema mlipuko wa bomu hilo ulikuwa na nguvu kuliko wa majaribio yaliyopita.
Mataifa mbalimbali yameshtushwa na jaribio hilo ikiwa ni pamoja na china, japan, urusi, na ufaransa, na kulitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya taifa hilo.