KOREA KASKAZINI NA KUSINI ZAKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO

 

 

Korea Kaskazini na Korea Kusini zimekubaliana kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu wiki ijayo. Hayo yametangazwa na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini ambayo imesema Korea Kaskazini imekubali mualiko wa kufanyika mazungumzo kati ya pande hizo mbili katika kijiji cha mpakani cha Panmunjom. Nchi hizo zitajadili uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi mwezi ujao na namna ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili