KOREA KASKAZINI YAFANYA GWARIDE KUBWA LA KIJESHI

 

Korea kaskazini imefanya gwaride kubwa la kijeshi mjini pyongyang  leo, katika kuonesha nguvu ilizonazo siku moja kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya olimpiki ya majira ya baridi nchini korea kusini.

Taifa hilo lenye silaha za kinyuklia la korea kaskazini linashiriki katika michezo hiyo ya olimpiki, na limetuma kundi la kutoa burudani, mamia ya washangiliaji wanawake, pamoja na dada wa kiongozi wa nchi hiyo kim jong un kwenda korea kusini.

wachambuzi wanasema hatua hiyo ya korea kaskazini huenda inaelekea katika kujitangaza kuwa taifa kamili la kinyuklia, na huenda likajaribu kudhoofisha vikwazo dhidi yake ama kuweka mgawanyiko baina ya korea kusini na mshirika wake marekani.