KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA KARIBU NA JAPAN

https://youtu.be/8O8yzb0pgVU

Korea kaskazini yarusha kombora karibu na japan

Waziri wa ulinzi wa japan amesema kuwa makombora yaliyorushwa na korea kaskazini yameanguka katika eneo la bahari la japan, takriban km 300 kutoka ufukwe wa kaskazini mashariki wa nchi hiyo.

Maafisa wa japan na korea kusini walithibitisha kuwa korea kaskazini imerusha makombora manne yaliyopigwa marufuku.

Bado hakuna uhakika kuhusu aina ya makombora yaliyorushwa na korea kaskazini, lakini mnamo miezi ya hivi karibuni nchi hiyo imefanya mfululizo wa majaribio ya makombora ya masafa mbalimbali.

Waziri mkuu wa japan shinzo abe amesema jaribio hilo linadhihirisha kuwa korea kaskazini imekuwa tishio.