KUACHA KUZIGEUZA EKA ZA SERIKALI KUWA MASHAMBA YA WANANCHI

 

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Ungja mhe: Idrissa Kitwana Mustafa amewasisitiza masheha na madiwani wa wilaya ya kati kuacha kuzigeuza eka za serikali kuwa mashamba ya wananchi na kukatwa viwanja vya ujenzi.

Akizungumza na madiwani, masheha, na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo mhe kitwana amesema  serekali imebaini hali hiyo ambayo inakwenda kinyume na  utaratibu  wa matumizi wa eka hizo na hupelekea  kuzuka  kwa migogoro ya ardhi.

Aidha amewataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato sambamba na kubuni vianzo vipya ili kuiwezesha serikali kutekeleza vyema mipango ya maendeleo

Nao watendaji hao wamemuelezea kaimu huyo  matatizo katika maeneo yao ikiwemo kutopatikana kwa uhakika wa huduma za kijamii za afya na maji safi.