KUANDAAA MKAKATI MADHUBUTI UTAKAOSAIDIA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA HADI LA SITA KUWEZA KUJUA KUSOMA ,KUANDIKA

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazni b rajab ali rajab amewataka walimu wakuu wa skuli za msingi kuandaaa mkakati madhubuti utakaosaidia wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita kuweza kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu ili kuinua kiwango cha elimu katika wilaya hiyo

Amesema kuwa anasikitishwa kuona wanafunzi katika wilaya yake wanafeli mitihani yao kutokana na kutojua kusoma ,kuhesabu na kuandika jambao ambalo linaizorotesha sekta ya elimu ambayo ndio tegemeo la taifa katika kuleta maendeleo

Akifunga mafunzo ya  rti ya tusome pamoja yaliyoshirikisha walimu wakuu wa skuli za msingi,wakaguzi pamoja na washauri mkuu huyo wa wialaya amesema sekta ya elimu katika wilaya ya kaskazini b bado inahitaji mkakati madhubuti hivyo ni vyema walimu wakuu wa kila skuli kuhakikisha skuli zao  zinahakiki  ufahamu wa mwanafunzi kabla ya kuwapeleka darasa jengine  ili kuleta hamasa ya kujituma katika masomo yao

Amesema kitendo cha walimu kuwaingiza madarasa mengine bila ya kuangalia ufahamu wa mwanafunzi darasani hautasaidia na badala yake utaendelea kuiweka wilaya hiyo katika hali mbaya kielimu

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru wizara ya elimu kwa kuandaa mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na wazazi wa wanafunzi ili kufikia lengo la mafunzo hayo kwa asilimia 75

Mafunzo hayo ya siku tano  ya rti tusome pamoja  yenye lengo la kusimamia majukumu ya walimu katika kumjenga mwanafunzi kuweza kujua kusoma,kuandika na kuhesabu yamefadhiliwa na marekani