KUANDALIWA KWA MPANGO MAALUMU WA KUPATIWA USHAURI NASAHA KWA WATU WANAOFANYA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

Kuandaliwa kwa mpango maalumu wa kupatiwa ushauri nasaha kwa watu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kunaweza kupunguza ongezeko la vitendo hivyo katika jamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya ustawi wa jamii duniani waziri wa kazi, uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto mh: moudline cyrus castico amesema mbinu hiyo inayotumika katika mataifa mengi yaliyoendelea itasaidia kudhibiti vitendo hivyo na kubadili tabia za watu wa aina hiyo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya ustawi wa jamii zanzibar (zaswa) said suleiman amesema ustawi wa jamii unajikita katika masuala ya haki za binaadamu, upatikanaji wa huduma stahiki za kijamii na usalama wa kila raia.

Siku ya ustawi wa jamii huadhimishwa kila ifikapo machi 21 ambapo ujumbe wa mwaka huu ni kuimarisha jamii na mazingira endelevu.