KUANZISHA DORIA SHIRIKISHI KATIKA GHUBA YA CHWAKA

 

idara ya maendeleo ya uvuvi imeandaa mpango maalum wa kuanzisha doria shirikishi katika ghuba ya chwaka lengo ni kusaidia ghuba hiyo kuzuwia vitendo vya uvuvi haramu.

mkurugenzi wa idara hiyo nd. mussa boud jumbe amesema hayo huko chwaka wakati akizungumza na kamati za uvuvi, na  masheha wa vijiji saba vinavyounganisha ghuba hiyo,ambapo amesema mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda rasilimali ya bahari.

amesema kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi lengo ni kuondoa  malalamiko  kwa baadhi ya wavuvi ambao wanadai wanaonewa pindi wanapokamatwa wakifanya vitendo vya uvuvi harau.

wakitoa michango yao juu ya kufanikisha mpango huo baadhi ya masheha na wenyeviti wameishauri idara kuweka mpango kazi mzuri ili kuweza kufanikisha jambo hilo  litasaidia kufanya kazi kwa pamoja na kuondosha malalamiko.

kikao hicho ni utekelezaji wa maombi ya kamati ya fedha,kilimo na biashara ya baraza la wawakilishi baada ya kufanya ziara hivi karibuni na kuitaka wizara ya kilimo,maliasili mifugo na uvuvi kukaa pamoja na wananchi ili kuweka ulinzi madhubuti utakaosaidia kuondosha malalamiko ya wavuvi.