KUANZISHWA KWA MABARAZA HAYO KUTAOANGEZA NGUVU SERIKALI

 

Serikali ya mkoa wa kaskazini pemba imesema uwepo wa mabaraza ya biashara katika ngazi ya mkoa kuwatatoa fursa kwa wafanyabiashara kukutana na kujadili changamoto zinazowakabilia na kuzitafutia ufumbuzi wake.

Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman akizungumza na ujumbe kutoka baraza la biashara la taifa zanzibar, amesema mabaraza hayo ni chachu ya kuongeza ajira kwa  vijana.

Amesema kuanzishwa  kwa mabaraza hayo kutaoangeza nguvu serikali na kupunguza malalamiko ya wafanyabiashara kwani yatarahisisha upatikanaji wa masoko.

Naye katibu mtendaji wa baraza la biashara la taifa Bakar Haji amezitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa ya uwepo na baraza hilo ili kuongeza mapato na ajira kwa vijana .

Katibu tawala mkoa huo ahmed khalid abdalla amesema baraza hilo ni chombo muhimu kitachowawezesha wafanyabiashara kupata ushauri wa kuyafikia masoko ya biashara zao.