KUBORESHA MAZINGIRA NA KUONGEZA IDADI YA MADAKTARI NA WAUGUZI

 

Waziri wa afya ,maendeleo ya jamii jinsia na watoto ummy mwalimu amefanya ziara katika  hospitali ya rufaa ya temeke jijini dar es salaam na kuahidi kulitafutia ufumbuzi suala la msongamano wa wagonjwa kwa kuboresha mazingira na kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi.

Akiwa hosptalini hapo waziri  ummy ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi ya wakina mama na vyumba vya upasuaji na kusikiliza changamoto na kuahidi kutafuta fedha zitakazowezesha kuongeza jengo la wodi ya wanawake na kuongeza vyumba vya upasuaji

Na kuhusu tatizo la msongamano wa wagonjwa waziri ummy amesema serikali itawaamisha madaktari bingwa kwa kuwatoa muhimbili ili kupunguza msongamano unaosababishwa na daktari mmoja kuhudumia wagonjwa wapatao mia tatu.

Nae mganga mfawidhi wa hosptali hiyo amani malima amemueleza waziri ummy kuwa msongamano huo unasababishwa  na upungufu  wa madaktari ulitokana  na tatizo la vyeti bandia hivyo ipo haja ya serikali kuongeza rasilimali watu ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

Baadhi ya wagonjwa waliofika hospitali hapa wameelezea  matarajio yao  ya kupata huduma ya matibabu kwa wakati wanapokwenda hosptalini hapo jambo ambalo imekuwa ni kinyume na matarajio yao.