KUBORESHA VIANZIO VYA MAPATO KWA KUFAYA TATHMINI YA MALI WANAZOZISIMAMIA

Manispaa wilaya ya mjini limeamua kuboresha vianzio vya mapato kwa kufaya tathmini ya mali wanazozisimamia ikiwemo ardhi na majengo ili kuweza kupata mabadiliko ya kimaendeleo katika mji wa zanzibar.
mstahiki meya wa baraza la manispaa abdul rahman khatib abdulrahman akizungumza katika kikao cha baraza kuu la madiwani kwa wilaya ya mjini amesema ni vyema kufanyika ka kwa tathmini i hiyo ambayo itatoa fursa ya kufahamu na kuweka kumbukumbu kwa watendaji itakayokuwa kila baada ya miaka mitatu
amesema kutokana na kuwepo kwa mali nyingi za kudumu katika manispaa ya mjini zinanasababisha mali hizo kuto kujulikana samani zake hivyo ni vyema kuwepo kwa mtaalamu wa kufanya tahmini ya mali hizo .
Akizungumzia kuhusiana na wafanya biashara na msongamano katika mji wa zanzibar amesema baraza la manispaa litajipanga upya kuhusiana na kuangalia mazingira mazuri ambayo yatawawezesha wafanya biashara wadogo wadogo ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
Badhi ya madiwani wakichia agenda za baraza hilo na kujadili agizo la serikali ya mkoa la kuondoshwa kawa soko la jioni la darajani na asilimia mbili ya makusanyo kwa maendeleo ya vijana wamesema
Mapema mkurugenzi wa baraza la manispaa hassan aboud serengea akiyataja baadhi ya malengo ya baraza hilo ni pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato na kusimamia huduma za usafi wa mazingira katika maeneo ya mji ambapo amesema jumla ya sh bilioni 2.3 zimekusanywa na baraza hilo kwa kipindi