KUBUNI MBINU ZA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

 

Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema inaendelea kuchukua juhudi katika kubuni mbinu za kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Waziri wa kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto  mh. Moudline castico, amesema hatua hiyo itaimarisha fursa za kujiajiri katika ajira zenye staha kwa wanawake.

Waziri castiko amefahamisha kuwa katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, lengo ni kutathmini mafanikio yaliopatikana na kubaini changamoto  katika kufikia maendeleo ya  kiuchumi, kielimu kiafya  pamoja na  kuimarisha ustawi wa wanawake.

Akizungumzia  suala la udhalilishaji kwa wanawake na watoto mh. Castico amesema wizara imeunda kamati maalum za kuhakikisha zinasimamia kwa pamoja katika kutokomeza vitendo hivyo