KUBUNI MBINU ZITAKAZOFANIKISHA MAPAMBANO YA KUKABILIANA NA VITENDO VYA DAWA ZA KULEVYA

Makamo wa pili wa rais balozi seif ali iddi ameshauri kubuniwa mbinu mpya zitakazofanikisha mapambano ya kukabiliana na vitendo vya dawa za kulevya hasa kwa za kuwabana wauzaji wanunuzi na wasafirishaji wa dawa hizo zanzibar.
Amesema mbinu hizo zitafanikisha mikakati ya kunusuru vijana wasiendelee kuathirika na dawa hizo ambao ni tegemeo kwa jamii.
Balozi seif ameeleza hayo katika hotuba yake iliyosomwa na waziri wa uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto mh. Moudlin castico katika uzinduzi wa taasisi ya kupambana na dawa za kulevya pamoja na mmong’onyoko wa maadili tanzania [green cresent community].
Amefahamisha kuwa mara nyingi wanaotumia dawa hizo ndio wanaojihusisha na vitendo vya wizi uhalifu vitendo udahalilishaji wa kijinisa na wengi wanaishia wanambukizwa na maradhi ya ukimwi hivyo ni vyema kuwepo na ushirikiano wa kukabiliana nazo.
Katika hotuba hiyo balozi seif ameishauri taasisi hiyo kuendeleza miradi itakayofanikisha pia juhudi za kusaidia matumizi sahihi ya teknolojia isitumike kinyume na maadili katika sehemu zote.
Katika taarifa ya uanzishwaji wa taasisi hiyo imeeleza kuwa wanatarajia kuanza awamu ya kwanza ya mradi utakaowasaidia vijana wanaoamua kuachana na dawa hizo pamoja na kuwashauri mbinu za kujiepusha kurejea matumiz ya dawa hizo.
Baadhi ya walioacha dawa za kulevya kwa muda wa miaka kadhaa wameipongoza serekali kwa juhudi wanayoichukua pamoja na kuelezea mafanikio waliyoyapata walipoaacha vitendo hivyo