KUCHIMBA MCHANGA MAENEO YASIYOKUWA RASMI NI UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini b  rajab ali rajab, amewataka wakaazi wa donge wanaojihusisha na shughuli ya kuchimba mchanga katika maeneo yasiyo rasmi kuwacha mara moja tabia hiyo, kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Amesema kitendo cha kuchimba mchanga katika maeneo yasiyokuwa rasmi ni miongoni mwa uharibifu wa mazingira ambapo serikali imekuwa ikichukua jitihada mbalimbali katika kudhibiti uharibifu huo ikiwemo kupanda miti katika maeneo ya mashimo yaliyochimbwa mchanga.

Nd rajab ameyasema hayo huko donge chechele katika heka ya bi  mtumwa ali ame,  ambae amelalamika kuchimbwa  mchanga  katika   heka yake na  kufanyiwa uharibifu  na baadhi ya wakaazi wa vijiji vya donge,  hali ambayo itasababisha uharibifu wa vipando vilivyomo katika heka hiyo ikiwemo minazi na miembe.

Amesema kuwa kitendo cha baadhi ya watu kuchimba mchanga katika eneo hilo ni kwenda kinyume na agizo la serikali hivyo  ni vyema wakazi hao wakachimba mchanga katika eneo lililotengwa ili kuepusha uharibifu wa mazingira

Msimami zi wa heka hiyo  bi mtumwa ali ame, amesema baadhi ya watu wanaochimba mchanga  wamekuwa wakimtishia amani ya maisha yake pale anapowaambia wasifanye vitendo hivyo au anapochukua hatua ya  kutowa taarifa serekalini.

Kwa upande wake sheha wa shehiya ya donge mbiji bwana abdalla machano haji, amesema hatua mbalimbali amekuwa akizichukua ikiwemo vikao na wazee wa vijiji hivyo lakini bado vitendo hivyo vinaendelea kujitokeza.