KUCHUKULIWA HATUA WATENDAJI WA ZECO AMBAO WATAFANYA UBADIRIFU WA FEDHA

Wajumbe wa baraza la waakilishi wameiyomba serikali kuwachukuli hatua watendaji wa shirika la umeme ambao watabainika kufanya ubadirifu wa fedha za serikali kwa maslahi yao binafsi.
Wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya aridhi maji nishati na mazingira wamesema shirika hilo limekuwa likiongoza wa matumizi mabaya ya fedha za umma na kusabisha kuitia hasara serikali.
Hata hivyo walitaka serikali ifanye utafiti sehemu za vijijini ili kuwabaini baadhi ya wafanyakazi wanaofanyakazi za shirika kwa maslahi yao na kutumia vifaa vya shirika hilo
Wakizungumzi suala la upatikana wa maji katika baadhi ya maeneo ya zanzibar wametaka wizara hiyo kutafuta mindombinu imara ili kuhakikisha wananchi wanaepukana na shida ya upatikana kwa muda mrefu.
wakizungumzia kuhusu migogorio ya ardhi wajumbe hao wamesema sheria ya ardhi iliyopo hivi sasa inaonekana kupitwa na wakati hivyo husabisha kuwepo kwa mrudikano wa kesi nyingi katika mahakama ya ardhi bila ya kupatiwa ufumbuzi.