KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MAGENDO NA MATUMIZI MABAYA YA BAHARI

Serekali ya mapinguzi ya zanzibar imo kuimarisha  miundo mbinu  ya ulinzi  na usalama  wa  bahari ili  kudhibiti   usafirishaji wa magendo  na  matumizi  mabaya ya bahari  yanayo kwenda kinyume  na sheria za nchi.

Waziri wa nchi  ofisi ya rais, tawala za mikoa,serekali za mitaa na idara maalum za smz  mh haji omar kheri   amesema hayo  katika hafla ya  uzinduzi wa boti mbili zenyeuwezo  za kukabiliana na vitendo viovu baharini ambazo zina milikiwa  na vikosi vya  zimamoto na uokozi, na kikosi maalumu cha kuzuwiya   magendo kmkm  katika bandari ya malindi .

Amesema  serekali inakusudia kurekebisha   sheria ili  kuviwezesha  vikosi hivyo  kutekeleza majukumu  yao kwa upana zaidi  kwa lengo  la kuimarisha uchumi  wa nchi.

Nae mkuu wa mkoa  wa mjini magharib mh ayoub mohammed  mahmoud  avitaka vikosi hivyo kuzitumia vyema   boti hizo ili kufikia   malengo  ya  serekali  ya kudhibiti vitendo vinavyo rudisha  nyuma  maendeleo ya taifa .