KUDHIBITI VITENDO VYA WIZI NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA

Wananchi wa shehia tatu za donge wameomba kusitishwa kwa huduma ya vibali vya ngoma kwa wananchi wa shehia hizo ili kudhibiti vitendo vya wizi na utumiaji wa dawa za kulevya katika shehia zao
Wakizungumza katika kikao maalum na mkuu wa wilaya ya kaskazin b wananchi hao wamesema baadhi ya wananchi wa shehia za donge mbiji,karange,na mnyimbi wamekuwa wakipiga ngoma bila kufuata taratibu walizoziweka na kusababisha kutokea kwa vitendo vya wizi na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na kuwepo kwa maingililiano ya watu kutoka maeneo mengine
Wamesema licha ya kuwepo na ulinzi shirikishi lakini bado vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza siku hadi siku na kusababisha wananchi hao kushindwa kupanda mazao ya aina yoyote kwani baadhi ya vijana hushirikiana na vijana wengine na kuiba mazao hayo yakiwa bado ni machanga
Mkuu wa wilaya ya kaskazini b issa juma ali amewataka wazee wa shehia hizo kuwa na utaratibu wa kukaa pamoja na vijana wao na kuwaeleza athari za wizi na ututumiaji wa dawa za kulevya ili kujenga taifa bora
Akizungumzia suala la wapiga ngoma ndugu issa amewataka wazee hao kuandaa orodha ya majina ya wahusika ili aweze kufanya mazungumzo ya pamoja na kufikia muafaka wa tatizo hilo