KUDUMISHWA UMOJA ULIOJENGEKA ILI TANZANIA ISONGE MBELE.

 

 

 

 

 

 

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, dk. John pombe magufuli amewaongoza watanzania kuadhimisha miaka 53 ya muungano wa tanganyika na zanzibar na kusisitiza kudumishwa umoja uliojengeka ili tanzania isonge mbele.

Amesema tanzania inajivunia  muungano huo kuendelea kudumu kwa kutokana na kuendelezwa dhana hiyo kama ilivyoasisiwa na viongozi waanzilishi marehemu mzee abaid karume na mwalimu julias kambarage nyerere.

Akiwahutubia wananchi katika  sherehe hizo zilizofanyika katika kiwanja cha jamhuri mkoani dodoma amesema watanzania wamedhihirisha kuwa muungano huo unadumu kwa kuwa ndio silaha ya kufikia maendeleo ya taifa.

Dk magufuli amesema serikali zote mbili za tanzania zimefanya jitihada kubwa ya kukuza uchumi, kukabiliana na matatizo ya umasikini, kuimarisha demokrasia, miundombinu pamoja na upatikanaji wa huduma za kijamii.

Ameeleza kuwa yeye pamoja na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt ali mohamed sheini kusimamia na kuulinda kwa nguvu zote huku akiahidi kuyapatia ufumbuzi matatizo mbalimbali ya muungano kwa kuondoa kero zilizopo kwa maslahi ya taifa.

Dk magufuli amesema kwa kuwa viongozi wote waliopita walioongoza serikali za tanzania watahakikisha wanafanya hivyo na yeyote atakaejitokeza kuutaka kuuharbu atachukuliwa  hatau.

Hivyo amesisitiza kuwa hawatakubali muungano huo kuvunjika katika utawala wake  na atakaefanya chohote atachukuliwa hatua za kisheria.

Mapema kabla ya kuanza kuwahutubia wanandhi dkt magufuli pamoja na mambo mengine alikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi na usalama sherehe hizo ambavyo baadae vilipita kutoa heshima zake katika jukwaa kuu la viongozi.

Maadhimisho hayo ni ya kwanza kufanyika mkoani dodoma mbali na gwaride pia maonesho ya ndege za angani na makomandoo wa jeshi la kujenga taifa yalifanyika ambapo viongozi mbali  walihudhuria akiwemo rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt ali mohamed shein.