KUFANYIWA HARAKA TARATIBU ZA KUZIRASIMISHA BANDARI BUBU ZA MANGAPWANI NA DONGE

Kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa serikali imependeza kufanyiwa haraka taratibu za kuzirasimisha bandari bubu za mangapwani na donge muwanda kutokana na kuwa tishio kubwa la uingizaji dawa za kulevya.
Kamati hiyo ambayo imeongozana na maafisa kutoka tume ya uratibu na kudhibiti dawa za kulevya na vikosi vya ulinzi imetembelea bandari za mangapwani na donge kuangalia hali halisi za bandari hizo ambazo zimekuwa zikitumika kwa shughuli mbali mbali za usafirishaji wa bidhaa ikiwemo ngombe.
Mwenyekiti wa kamati hiyo mh. Omar seif abeid amesema kutokana na mazingira ya bandari hizo iwapo hakutakuwa na ushirikiano, pamoja na kutambulika rasmi inaweza kuwa mlango mkubwa wa kuingiza dawa hizo kw kukosekana udhibiti.
Wakitoa maoni yao wajumbe wa kamati hiyo pamoja na maafisa wengine wamesema wamewataka masheha kuwatambua wahamiaji haramu katika shehia zao na kufuatilia nyendo zao ili kuwabaini iwapo hawajishirikishi katika biashara hizo.
Katika hatua nyengine kamati hiyo imezungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini unguja ambapo mku wa mkoa mh. Vuai mwinyi ametaka wananchi kushirkiana ili kupambana na vita hivyo licha ya chngamaoto zilizopo.